UKATOLIKI NI FAHARI YANGU
Na: JOSEPH JS SIKAZWE
DODOMA - 2025
Utangulizi : (I&II) Ukatoliki ni fahari yangu, (W) najivunia kuwa Mkatoliki Ukatoliki, Ukatoliki fahari yangu najivunia x 2//
Kibwagizo: (IV) Kanisa moja Takati - fu (W) Katoliki la Mitume, (III) ni moja Kani - sa Katoli - ki, (W) fahari yangu najivunia Kanisa hili.
Mashairi:
1. (III&IV): Natembea nao Ubatizo ni mmoja Mtakatifu (I&II): Nilio batizwa ni kwa jina la Utatu Mtakatifu – (W) Ukatoliki Neema nyingi najivunia.
Kibwagizo (IV): Kanisa moja ………
2. (III&IV): Ni Kanisa Kuu Takatifu alilioanzisha Kristo (I&II): Na analilinda kwa nguvu zake Roho Mtakatifu - (W) Ukatoliki Neema nyingi najivunia.
Kibwagizo (IV): Kanisa moja ………
3. (III&IV): Alimwambia Simon Petro wewe ndiwe mwamba ni mwamba, (I&II): Na juu ya mwamba mwamba huo nitajenga Kanisa langu - (W) Ukatoliki Neema nyingi najivunia.
Kibwagizo (IV): Kanisa moja ………
4. (III&IV): Mkatoliki furahi sana kwani wewe upo salama, (I&II): Umwambie Mungu asante kwa neema ya Ukatoliki - (W) Ukatoliki Neema nyingi najivunia.
Kibwagizo (IV): Kanisa moja ………
Hitimisho
(III&IV) : Ukatoliki ni fahari yangu – (W) najivunia Ukatoliki fahari yangu
Ukatoliki ni furaha yangu – (W) najivunia Ukatoliki furaha yangu
(I&II) : Mkatoliki (W) simama, (I&II) : na utembee (W) Imara, (I) kwani
1. (W) - upo kwenye Safina imara.
2. (W) – upo ndani ya chombo imara
3. (W) - upo juu ya mwamba imara.
4. (W) – upo kwa mchungaji wa kweli.
5. (W) - upo kwenye mikono ya kweli.
6. (W) – upo kwenye imani ya kweli.
No comments:
Post a Comment